Ceuta
Mandhari


Ceuta (tamka: the-uta; kwa Kiarabu: سبتة sabta) ni mji wa Kihispania kwenye pwani ya Mediteranea ambao upande wa bara unazungukwa na eneo la Moroko. Ceuta iko karibu na mji wa Tetouan upande wa Moroko. Umbali na Hispania ni km 21 kuvuka mlango wa bahari wa Gibraltar.
Pamoja na mji wa Melilla ni sehemu ya Hispania na Umoja wa Ulaya kisiasa , lakini kijiografia ni sehemu ya Afrika. Moroko inadai ni sehemu ya eneo lake la kitaifa.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Ceuta ina wakazi 75.276 katika eneo la km² 18.5. Karibu nusu ni Wazungu/Wakristo na nusu ya pili ni Waberber-Waarabu/Waislamu.