Dhambi
Mandhari
Dhambi (kutoka Kiar. ذنب dhanaba kukosa, kutenda dhambi au jinai[1]) ni kosa la kiumbehai mwenye hiari dhidi ya uadilifu unaompasa.
Inaweza kufanyika kwa mawazo, maneno, matendo na kwa kutotimiza wajibu.
Maadili yanamuelekeza binadamu katika kutambua dhambi ni zipi pamoja na madhara yake.
Kwa kawaida dini zinahusianisha kosa hilo na Mungu aliye asili ya uadilifu, kwa kuwa ndiye aliyeumba viumbe vyote na kuvielekeza