Hezi
Mandhari
Hezi, pia hertz , kifupi Hz ni kipimo cha SI kwa marudio ikitaja rudio 1 kwa sekunde 1. Inatumiwa hasa kwa kutaja tabia ya mawimbi kama wimbisauti au mawimbi sumakuumeme za redio na pia marudio katika mitambo kwa mfano kompyuta.
Kipimo hiki kilipokea jina lake mwaka 1930 kwa heshima ya mwanafizikia Mjerumani Heinrich Hertz aliyekuwa mtaalamu wa kwanza wa kuonyesha kuwepo kwa mawimbi sumakuumeme.
Ngazi za Hz
[hariri | hariri chanzo]Kipimo cha Hz hutumiwa mara nyingi kwenye ngazi zifuatazo:
| Jina | Kifupi | Zaomtiririko | Marudio/sekunde | Mifano |
|---|---|---|---|---|
| Kilohezi (Kilohertz) | kHz | Marudio 1000 kila sekunde. Sauti za juu sana katika muziki zina kHz kadhaa hadi 20 kHz. | ||
| Megahezi (Megahertz) | MHz | marudio milioni 1 kila sekunde. Vituo vya redio vya FM hutumia mawimbi ya sumakuumeme yenye marudio mnamo 100 MHz. | ||
| Gigahezi (Gigahertz) | GHz | marudio bilioni 1 kila sekunde. CPU za kompyuta huwa na marudio katika kiwango cha GHz kadhaa. | ||
| Terahezi (Terahertz) | THz | marudio triliardi 1 kila nukta. Nuru huwa na marudio kwenye kiwango cha 1000 THz. | ||
| Petahezi (Petahertz) | PHz |