Kelvini
Mandhari

Kelvini ni Kizio cha SI kwa halijoto. Alama yake ni K.
Kiwango chake kinaanza kwenye sifuri halisi (= -273.15 °C) pasipo mwendo wowote wa molekuli. Kizio kimoja cha Kelvini ni sehemu ya 1/273.16 ya tofauti kati ya sifuri halisi (=0 K) na kiwango utatu cha maji (+0.01 °C).
Skeli ya Kelvini ililinganishwa na skeli ya selsiasi yaani kizio kimoja cha Kelvini ni sawa na kizio kimoja cha Selsiasi.
Skeli ya Kelvini haina namba hasi (-) kwa sababu hakuna hali chini ya 0 K.
Jina limetokana na mwanafizikia Mwingereza William Thomson aliyekuwa na cheo cha Lord Kelvin (1824–1907).
| Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu |